Kamati ya
Usajili ya Simba, imefanya kweli kwa kuwabakiza wachezaji wake wawili, Said
Ndemla na Hassan Isihaka.
Isihaka ambaye
ni nahodha wa Simba, ilielezwa alikataa kusajili kwa madai nataka dau nono
zaidi.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia hans Poppe amesema tayari wamemalizana na
wachezaji hao kwa kuwaongezea mikataba ya miaka mitatu kila mmoja.
“Wote wawili,
kila mmoja tumemuongezea mkataba wa miaka mitatu,” alisema Hans Poppe.
“Tunaendelea
kufanya mazungumzo na wengine ambao tunahitaji wabaki. Kidogo tunafanya mambo
yetu hatua kwa hatua.”
Simba tayari
imeanza kufanya usajili wa kuboresha safu yake ya kiungo lakini walichopanga
kwanza ni kuwabakiza wachezaji wanaowataka.
Hans Poppe
ndiye mwenyekiti wa kamati hiyo na makamu wake ni Kassim Mohammed Dewji.
0 COMMENTS:
Post a Comment