July 26, 2021

 UONGOZI wa Yanga umewashukuru mashabiki wao ambao walijitokeza kwa wingi jana kuipa sapoti timu hiyo.



Ni katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika,  Kigoma mwisho wa reli. 


Licha ya jitihada za wachezaji kusaka ushindi ngoma ilikuwa nzito kwa Yanga kwa kuwa walikubali kuokota bao moja nyavuni. 


Ilikuwa kupitia kiungo mkabaji, Taddeo Lwanga aliyepachika bao hilo kwa bichwa dakika ya 76 na lilidumu mpaka mwisho wa mchezo. 


Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Yanga wameandika kwamba shukrani kwa mashabiki waliojitokeza kuipa sapoti timu ya Wananchi.


Tayari kikosi kimerejea Dar es Salaam wakiwa na medali za mshindi wa pili na taji limeelekea kwa watani zao Simba ambao nao waharejea Dar.

12 COMMENTS:

  1. Duuh hata kusema hongera kwa watani zetu hakuna, wivu utatuua

    ReplyDelete
  2. Timu ya wananchi.... usemi huu ni ktk kutafuta huruma kutoka kwa hao wanaoitwa wananchi, janja ya nyani.

    ReplyDelete
  3. Mashabiki uchwara bhana!! Ile pongezi aliyotoa hersi ilikuwa ya Mo au huwa hamsomi?

    ReplyDelete
  4. Mashabiki ndio kila kitu. Kucheza 10 kwa zaidi ya dk 45 sio kazi ndogo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Simba ishawahi kucheza pungufu na utopolo na tumewagomga mara zote

      Delete
    2. Simba ishacheza zaidi ya dk 70, ikafanya comeback na kushinda 2-1 dhidi ya yanga

      Delete
  5. Mikia sikuzo wanawivu na maendeleo ya Yanga, habari inawahusu Yanga negative comments za nn?
    Kwann msizungumzie migogoro yenu na Manara?

    ReplyDelete
  6. Hakuna mgogoro na Manara ila alitafuta attention kwa audience. Tukavutika na kusahau mechi

    ReplyDelete
  7. Ukizaa Mwanao akapenda Simba hata ukimpeleka Chuo Kama Harvard bado utamtafutia tuisheni,wengi mapunguani

    ReplyDelete
  8. Mambo achezaji watambue umuhimu wa mechi za fainali inavutu vingi sana kadi ya mukoko imetugharibu kuxhindwa kushambulia hatimae kujilinda zaidi big up wachezaji na benchi la ufundi kwa kocha huyu watalia sana

    ReplyDelete
  9. Siyo mbaya mbona so tuliwafunga huo ndio Mpira tusipende kwenda uwanjani na matokeo hongera wachezaji wetu mmepambana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic