May 24, 2018


Taarifa zinaeleza kuwa Shirikisho la Soka Barani Africa (CAF) limefanyia mabadiliko ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika iliyokuwa ikifanyika kwa mwezi Februari hadi Novemba.

Mabadiliko hayo yanaonesha kuwa ratiba ya michuano hiyo itakuwa inafanyika mwezi Mei mpaka Agosti badala ya ilivyokuwa imezoeleka.

Imeelezwa sababu kubwa iliyopelekea kubadilishwa kwa ratiba hiyo ni kuendana  sambamba na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA Champions League) ambayo huchezwa wakati ligi zinaendelea.

Kwa msimu ujao mashindano hayo yataanza mwezi Disemba mpaka Mei ikiwa ni kabla ya mabadiliko tajwa hapo juu kuanza kutumika rasmi.

Uamuzi huo umekuja wakati klabu ya Simba hapa nchini ikiwa tayari imeshakata tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Wakati huo mwakilishi wa Kombe la Shirikisho Afrika bado hajapatikana ambapo baada ya mchezo wa fainali ya Azam Sports Federation CUP kati ya Singida United na Mtibwa Sugar ndiyo unaotarajiwa kupigwa siku kadhaa zilizosalia utatoa rasmi timu itakayoshiriki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic