May 16, 2015


Kocha Piet de Mol raia wa Ubelgiji ndiye atachukua mikoba ya Goran Kopunovic.

De Mol anatarajia kutua nchini kati ya Mei 21 hadi 23 tayari kumaliza na uongozi wa Simba na mara moja ataanza kazi.
Uongozi wa Simba umefikia uamuzi huo baada ya Kopunovic kutaka dau kubwa sana.

Kopunovic aliondoka mapema wiki hii kurejea kwao huku akiwa ameshindwa kuelewana na uongozi wa Simba.

MSerbia huyo anayeishi nchini Hungary alitaka kulipwa dola 50,000 (sh milioni 100) kama ada ya usajili.

Pia alitaka kupewa mshahara wa dola 14,000 ambazo zingemfanya kuwa kocha ghali zaidi nchini.

Simba iliamua kubadili uamuzi wa kubaki naye na kufanya mazungumzo na Mbelgiji huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic