Kocha
Piet de Mol raia wa Ubelgiji ndiye atachukua mikoba ya Goran
Kopunovic.
De Mol
anatarajia kutua nchini kati ya Mei 21 hadi 23 tayari kumaliza na uongozi wa Simba na mara moja ataanza
kazi.
Uongozi
wa Simba umefikia uamuzi huo baada ya Kopunovic kutaka dau kubwa sana.
Kopunovic
aliondoka mapema wiki hii kurejea kwao huku akiwa ameshindwa kuelewana na
uongozi wa Simba.
MSerbia huyo
anayeishi nchini Hungary alitaka kulipwa dola 50,000 (sh milioni 100) kama ada
ya usajili.
Pia
alitaka kupewa mshahara wa dola 14,000 ambazo zingemfanya kuwa kocha ghali
zaidi nchini.
Simba
iliamua kubadili uamuzi wa kubaki naye na kufanya mazungumzo na Mbelgiji huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment