‘Uswahili’ wamponza
Kaswahili, Yanga yafungua kesi mahakamani, TFF
Uongozi wa Klabu ya Yanga
umetangaza kumfungulia mashtaka mahakamani na kumfikisha katika kamati ya
nidhamu ya TFF, mdau wa soka Bw Fransic Kaswahili kwa kitendo cha kutangaza kwenye
vyombo vya habari uwepo wa uchaguzi mkuu wa klabu hiyo, jamboa ambalo uongozi
umekanusha.
Mei 14, 2015 Kaswahili
ambaye alijitambulisha kama katibu wa kamati ya uchaguzi wa Yanga, alisambaza
taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa kutakuwa na uchaguzi mkuu ambao
utafanyika July 12, mwaka huu huku fomu za kugombea zitaanza kutolewa Mei 17,
mwaka huu katika makao makuu ya klabu.
Akizungumza katika mkutano
na waandishi wa Yanga, Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amewaomba wanachama
na mashabiki wa Yanga kupuuzia tangazo la ndg Kaswahili na kwamba wameamua
kumfikisha kwenye kamati ya maadili ya TFF kwani wameona kumvua uanachama haitatosha,
hivyo wamemua kuanzia kwa TFF.
Aidha, wameamua kumfungulia
mashtaka ya jinai na madai makosa yafuatayo:
i)
Taarifa
yake ilikuwa ni uchochezi wa kuvuruga amani ndani ya klabu hiyo kwa kuitisha
uchaguzi batili, akiwa si kiongozi wa Yanga.
ii)
Kuidhalilisha
klabukwa kutumia jina lake na kujiita katibu wa kamati ya uchaguzi wakati
akijua fika si kiongozi wa kamati yoyote na mbaya zaidi si mwanachama hai kwa
kile alichoeleza Dk Toboroha kuwa hajalipia kadi ya uanachama tangu 2012, hivyo
kitendo cha kutolipia kadi yake baada ya ya miezi sita, kisheria unakuwa si
mwanachama hai, hivyo hata uchaguzi ungekuwepo, bado asingeruhusiwa kupiga kura
mpaka achukue kadi mpya kwa wazabuni wao; CRDB na Posta Bank.
iii)
Kuzungumzia
masuala ya klabu bila kuwasiliana na sekritariet husika
iv)
Ilikuwa
ni njia ya kuwatapeli wanachama wa Yanga kwa kutangaza bei za fomu za uchaguzi
huo BATILI.
Hata hivyo Kasawahili alikuwa
amepewa nafasi ya kukanusha taarifa zake kupitia ‘media’ alizowapa taarifa hiyo
kufikia leo 6:00 mchana, lakini akashindwa, hivyo suala lake linatua TFF na mahakamani.
Mkutano wa waandishi ulifanyika saa 7:00 ili usubiri taarifa yake ya kukanusha.
DK Tiboroha amefafanua kuhusu Kaswahili
aliwahi kuwa katibu wa kamati ya uchaguzi katika utawala uliopita kabla ya kamati
hiyo kuvunjwa mwaka jana mwezi Machi, kwa ajili ya kupisha uchaguzi mkuu mwingine
ambao ulikuwa ufanyike mwaka jana, lakini kwa ridhaa ya wanachama wakauongozea
muda uongozi wa Manji kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi, Alex Mgongolwa muda wowote atatangaza ratiba ya uchaguzi mkuu.
Aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya
uchaguzi utawala uliopita, Mh. Jaji Mkwawa amejitoa katika timbwili la Kaswahili.
0 COMMENTS:
Post a Comment