May 13, 2015

Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amewasili nchini kwao Burundi ambako mipaka ya nchi hiyo imefungwa.


Mipaka imefungwa baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kupinduliwa na wanajeshi wa nchi hiyo. Mapinduzi hayo yanaongozwa na Meja Jenerali, Godefroid Niyombar.

MEJA JENERALI NIYOMBAR
Ingawa kumekuwa na taarifa ya waliomuondoa Nkurunziza kufunga mipaka yote na kuushikilia uwanja wa ndege wa nchi hiyo.

Lakini Tambwe hayuko Bujumbura imeelezwa yuko nyumbani kwao ambako si mbali sana na mpaka wa Tanzania.

Nkurunzinza amepinduliwa akiwa nchini kwa ajili ya mkutano kujadili kuhusiana na suala la yeye kutaka kugombea mara ya tatu.


Burundi imeingia kwenye mgogoro na maandamano makubwa baada ya Nkurunzinza kulazimisha kugombea urais kwa mhula wa tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic