Washindi
wa simu za kisasa za Lumia Microsoft kutoka nchi za Kenya, Uganda na Tanzania
watakula ‘bata’ ya kutosha katika jiji la Cape Town nchini Afrika Kusini kwa siku tatu.
Mshindi kutoka
Tanzania, Richard Edward Mtango, Isaac Kinyera wa Uganda na Philip Mwaura kutoka
Kenya watajumuika pamoja katika mji huo maarufu kama “Mother City”.
Yote hayo yalikuwa
ni kupitia ile kampeni ya Make it Happen na zawadi zimekuwa zikitolewa kwa
washindi mbalimbali.
Lengo ni
kuwaonyesha watu mbalimbali ubora wa simu hizo za kisasa zaidi ambazo
zinamuwezesha kupata kila anachotaka.
Programu kadhaa
katika simu hizo zinaweza kuwasaidia wanamichezo kupata kila wanachohitaji na
kwa ulahisi zaidi kutokana na ubora wa simu hizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment