Pamoja na kuonekana ni timu ‘mchekea katika nne zilizoingia nusu
fainali, Juventus imefanikiwa kutonga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Juventus imeingia fainali na sasa itacheza dhidi ya Barcelona Juni 6, mwaka huu jijini
Berlin, Ujerumani.
Imetinga fainali baada ya kuing’oa Real Madrid kwa jumpa ya mabao 3-2 katika
mechi ya nusu fainali ya pili iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mechi hiyo iliisha kwa sare ya bao 1-1 baada ya Ronaldo kuanza kuifungia
Madrid kwa penalti kabla ya Alvaro Morata kusawazisha katika kipindi cha pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment