Mshambuliaji
wa Yanga, Amissi Tambwe amewasili nchini kwao Burundi ambako mipaka ya nchi
hiyo imefungwa.
Mipaka
imefungwa baada ya Rais Pierre Nkurunzinza kupinduliwa na wanajeshi wa nchi hiyo. Mapinduzi
hayo yanaongozwa na Meja Jenerali, Godefroid Niyombar.
MEJA JENERALI NIYOMBAR |
Ingawa
kumekuwa na taarifa ya waliomuondoa Nkurunziza kufunga mipaka yote na
kuushikilia uwanja wa ndege wa nchi hiyo.
Lakini
Tambwe hayuko Bujumbura imeelezwa yuko nyumbani kwao ambako si mbali sana na
mpaka wa Tanzania.
Nkurunzinza amepinduliwa akiwa nchini kwa ajili ya mkutano kujadili kuhusiana na suala la yeye kutaka kugombea mara ya tatu.
Burundi
imeingia kwenye mgogoro na maandamano makubwa baada ya Nkurunzinza kulazimisha
kugombea urais kwa mhula wa tatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment