Hatimaye mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amekamilisha
ndoto yake ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Frolence Nakalegga .
Sherehe hiyo imefanyika jijini Kampala, Uganda jana kwa
Okwi kuhitimisha shughuli hiyo.
Awali Okwi aliwahi kufunga ndoa ya kimila kwa ajili ya
kumtambulisha mpenzi wake huyo kwa wazazi wake.
Lakini jana ilikuwa ni funga kazi huku watu mbalimbali
wakiwemo maofisa wakubwa wa jeshi wakihudhuria.
Kivutio zaidi kilikuwa ni mpambe wake katika shughuli hiyo
kuwa ni mshambuliaji nyota wa zamani wa Yanga, Hamis Kiiza.







0 COMMENTS:
Post a Comment