July 6, 2015

SIKU MASHABIKI WALIPOMPOKEA...
Mshambuliaji mpya wa Simba, Hamis Kiiza anaamini kikosi chake kipya kitabeba ubingwa wa Bara.


Kiiza alitemwa na Yanga msimu uliopita na aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi hicho Mbrazili, Marcio Maximo katika kipindi cha dirisha dogo baada kuonekana hafai, nafasi yake ikachukuliwa na Genilson Santana ‘Jaja’.

Lakini Simba ambao ni watani wa jadi, wameamua kumrejesha Kiiza kwenye Ligi Kuu Bara kwa kumpa mkataba wa miaka miwili.

Kiiza amesema mbali na kuja kuthibitisha ubora wake, pia ni kuhakikisha Simba inarejesha heshima yake.
Kiungo huyo mwenye kasi na kuitambua vizuri milingoti mitatu ya wapinzani, alisema kuwa atapambana kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa na kucheza michuano ya kimataifa.

“Kuna mambo mawili nimepanga kuyafanya nikiwa na timu yangu mpya, kwanza ni kuhakikisha naisaidia kuipa ubingwa na pili kuthibitisha ubora wangu,” alisema Kiiza.

Kiungo huyo ambaye tayari mashabiki wa Simba wamembatiza jina la Aguero, aliongeza kuwa kwa kuwa ni mzoefu katika ligi, haitampa shinda huku akitambia usajili wa timu hiyo ambao unaendelealea kufanywa.


“Hakuna kitu ambacho nilikuwa nakitamani kama kucheza timu moja na Okwi (Emmanuel), kule Uganda huwa tunakutana muda mfupi lakini sasa tutakuwa klabu moja, mashabiki wa Simba watarajie furaha tu,” alisema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic