SIKU MASHABIKI WALIPOMPOKEA... |
Mshambuliaji mpya wa Simba, Hamis Kiiza anaamini kikosi chake
kipya kitabeba ubingwa wa Bara.
Kiiza alitemwa na Yanga msimu uliopita na aliyekuwa kocha mkuu wa
kikosi hicho Mbrazili, Marcio Maximo katika kipindi cha dirisha dogo baada
kuonekana hafai, nafasi yake ikachukuliwa na Genilson Santana ‘Jaja’.
Lakini Simba ambao ni watani wa jadi, wameamua kumrejesha Kiiza
kwenye Ligi Kuu Bara kwa kumpa mkataba wa miaka miwili.
Kiiza amesema mbali na kuja kuthibitisha ubora wake, pia ni
kuhakikisha Simba inarejesha heshima yake.
Kiungo huyo mwenye kasi na kuitambua vizuri milingoti mitatu ya
wapinzani, alisema kuwa atapambana kuhakikisha timu hiyo inachukua ubingwa na
kucheza michuano ya kimataifa.
“Kuna mambo mawili nimepanga kuyafanya nikiwa na timu yangu mpya,
kwanza ni kuhakikisha naisaidia kuipa ubingwa na pili kuthibitisha ubora
wangu,” alisema Kiiza.
Kiungo huyo ambaye tayari mashabiki wa Simba wamembatiza jina la
Aguero, aliongeza kuwa kwa kuwa ni mzoefu katika ligi, haitampa shinda huku
akitambia usajili wa timu hiyo ambao unaendelealea kufanywa.
“Hakuna kitu ambacho nilikuwa nakitamani kama kucheza timu moja na
Okwi (Emmanuel), kule Uganda huwa tunakutana muda mfupi lakini sasa tutakuwa
klabu moja, mashabiki wa Simba watarajie furaha tu,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment