August 29, 2015


Licha ya mvua kubwa ambayo ilikuwa ikinyesha jana saa 3 asubuhi, hiyo haikuwazuia Simba kufanya mazoezi huku ‘wakiloa’ na kocha Dylan Kerr alisema: “Hapa kazi tu.”

Simba ipo visiwani hapa ikiwa imeweka kambi ikijiandaa na Ligi Kuu Bara ambayo itaanza rasmi Septemba 12, mwaka huu na jana ilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa wa Amaan uliopo mjini Unguja huku ikinyeshewa na mvua.

Kikosi hicho kilikuwa kikifanya mazoezi aina tofauti tayari kwa kujiandaa na ligi hiyo ambapo kitafungua pazia dhidi ya African Sports ya Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani.


Kocha Mkuu wa Simba, Dylan Kerr, alionekana akiwafanyisha mazoezi ya pasi wachezaji wake pamoja na kupiga mashuti ya mbali huku mvua ikinyesha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic