August 29, 2015


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limetuma salam za rambi rambi kwa Chama cha Soka mkoa wa Pwani (COREFA) kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu wa FIFA na kamishina wa TFF, Gilbert Mando kilichotokea jana mjini Bagamyoyo.

Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini, TFF inawapa pole familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.
Marehemu Gilbert Mando alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya figo mpaka umauti ulipomfika jana jioni nyumbani kwake eneo la Bong’wa Bagamoyo, taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwa marehemu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic