August 29, 2015

KAMUSOKO

Kiungo wa Simba, Justice Majabvi, raia wa Zimbabwe, kufungua mdomo wake na kutamka kuwa kiungo wa kati wa Yanga, Thabani Kamusoko ni hatari sana!

Kamusoko ambaye ana rasta, anatajwa kuwa bora katika safu ya kiungo mkabaji, huku kiwango katika mchezo na Azam wiki iliyopita na kutwaa taji la Ngao ya Jamii, kikimfanya awe miongoni mwa viungo wakabaji watakaotisha msimu ujao.

Majabvi alisema anaufahamu vyema uwezo wake tangu wakiwa nchini kwao Zimbabwe huku sifa kuu akisema ni umakini katika kukaba.
MAJABVI
“Thabani namjua kwa kiasi, ni kiungo mzuri. Yupo makini sana katika kukaba, hapotezi mipira hovyo, pia anajua kuichezesha timu. Kwa kifupi atawasaidia katika safu ya kiungo,” alisema Mzimbabwe huyo.


Hata hivyo, kizingiti kikubwa kwa Kamusoko ni uwepo wa Said Juma Makapu, Salum Telela na Mbuyu Twite ambao pia huitendea haki namba sita.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic