February 9, 2016

NGOMA AKIWA MAZOEZINI...

Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma anajua kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara ni ngumu hasa, lakini anachoahidi ni kupambana.

“Ni ligi ngumu, una ushindani. Mabeki hawataki kufungwa, lakini mimi ni mshambuliaji, ninatakiwa kufunga, hivyo lazima nifunge,” alisema Ngoma.

Ngoma raia wa Zimbabwe, sasa ana mabao 10 katika ligi hiyo na anahitaji kufunga zaidi licha ya kwamba amekuwa mmoja wa washambuliaji wanaobanwa vilivyo na mabeki.

Pamoja na kufunga, Ngoma amekuwa ni chachu ya kutengeneza mabao au kuwachosha mabeki wa timu pinzani.


Mzimbabwe huyo ni mbishi na asiyekubali kushindwa na amekuwa akipambana vilivyo na mabeki wakatili wa timu pinzani za Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic