February 9, 2016




Na Saleh Ally
Hadithi ya safu za ulinzi za Yanga, Azam FC na Simba inachekesha sana na hii inaonyesha kwamba katika soka, kuna mambo mengi sana ya kufanya ili kufikia mafanikio.

Hakuna asiyejua safu ya ulinzi ya Yanga ina wachezaji wa kulipwa au wazoefu kabisa kama Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani. Pia kuna Vicent Bossou, mchezaji wa kulipwa kutoka nchini Togo na wakati mwingine anasaidiana na Mbuyu Twite kutoka Rwanda mwenye asili ya DR Congo pamoja na Mzimbabwe, Thabani Kamusoko.

Upande wa Azam FC, kuna mtu anaitwa Serge Wawa raia wa Ivory Coast,Racine Diouf raia wa Mali. Wazalendo Aggrey Moriss, Said Morad na David Mwantika.

Ukipiga hesabu za kawaida kwa maana ya usajili au malipo, wale wa Azam FC na Yanga watakuwa ni ghali zaidi lakini hata uzoefu, bado wale wa Yanga na Azam FC wanaoneka kuwa wakongwe zaidi.

Kwa upande wa Simba, safu hiyo zaidi inaongozwa na watu hawa wanne, ambao wote ni wazalendo kasoro mmoja. Sitamweka kiungo Justuce Majabvi anayeonekana kutokuwa fiti sana hasa katika mechi za mwisho.

Lakini Mganda, Juuko Murshid anashirikiana na wazelando, Abdi Banda, Hassan Isihaka na Jonas Mkude ambao ni wachezaji makinda wanaoonekana kuwa na uwezo mkubwa katika ulinzi.

Katika mechi 18, Simba imefungwa mabao 10 sawa na Azam FC ambayo imecheza mechi 16. Kuna uwezekano wa beki ya Azam FC ambayo ni ghali na ya wakongwe ikaruhusu mabao zaidi katika mechi zake mbili zaidi za viporo.

Yanga yenyewe imefungwa mabao 9 tu baada ya mechi 18, ni tofauti ndogo sana na Simba yenye vijana wengi, pia wachezaji wasio ghali sana kama wale wa Yanga ambayo safu yake ya ulinzi ina wageni watatu.


Kama Simba watawahasisha vizuri vijana wao nao wakaendelea kujituma vilivyo, huenda wakawa safu bora ya ulinzi msimu katika kulinganisha na safu nyingine za wapinzani wao wakubwa ambao ni Yanga na Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic