February 9, 2016


Beki wa kati na nahodha wa yanga, Nadir Ally Haroub amesema anarejea lakini hana wasi hata kidogo kwamba anahitaji muda ili kuwa vizuri.

Cannavaro ameiambia SALEHJEMBE kwamba alikuwa na maumivu makali kwenye mguu uliokuwa majeruhi, lakini sasa anajisikia vizuri.

“Nimefanya mazoezi ya peke yangu gym na hata kukimbia barabarani na uwanjani, sasa naona niko vizuri.

“Sina hofu hata kidogo kwamba nikirudi ninahitaji muda. Ninaweza nisiwe vizuri sana na hofu ya kutoka kwenye majeraha, lakini najua nicheze vipi,” alisema.

Cannavaro alitarajia kuanza mazoezi rasmi na wenzake ikiwa ni hatua ya kwanza ya kurejea kikosini baada ya kukaa nje kwa zaidi ya wiki tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic