April 29, 2016




KAMATI YA RUFAA YA NIDHAMU
Kikao cha Kamati ya Rufaa ya Nidhamu kitafanyika Jumamosi Aprili 30, 2016 kuanzia saa 4.00 asubuhi kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kitajadili rufaa za timu, makocha, viongozi na wachezaji waliokata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Nidhamu baada ya kamati hiyo kuwatia hatiani na kuwaadhibu kwa makosa ya kupanga matokeo ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza.

Rufaa zitakazojadiliwa kwenye kikao hicho ni za:

     1. Timu ya Geita Gold
  1. 2. Choki Abeid ambaye ni Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Geita Gold FC
  2. 3. Denis Richard Dioniz - Kipa wa Geita Gold
  3. 4. Fatel Rhemtullah – Katibu wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Tabora
  4. 5. Saleh Mang’ola – Mwamuzi wa Soka wa Mkoa wa Dodoma
  5. 6. Timu ya Soka ya Polisi Tabora
  6. 7. JKT Oljoro Fc ya Arusha 
  7. 8. Yusufu Kitumbo – Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora.
MECHI ZA LIGI BARA 
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendeleo mwishoni mwa wiki hii kwa michezo sita itakayofanyika kwenye viwanja mbalimbali nchini.

Mabingwa wanaotetea taji hilo, Yanga ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa Toto Africa katika mchezo utakaofanyika Uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza huku Coastal Union ikipambana na African Sports kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Mechi nyingine zitakuwa ni kati ya Mwadui FC watakaokuwa wenyeji wa Stand United kwenye Uwanja wa Mwadui, Shinyanga wakati Mbeya City watakuwa wageni wa Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu, Mvomero mkoani Morogoro na katika Dimba la Sokoine jijiji Mbeya Tanzania Prisons itaumana na JKT Ruvu katika mfululizo wa mechi za ligi hiyo.

Jumapili Simba itaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Michezo yote itaanza saa 10.000 jioni na kurushwa moja kwa moja na vituo vya televisheni ya Azam.

IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic