April 29, 2016


MSEMAJI WA TFF, ALFRED LUCAS MAPUNDA

Kikao cha Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kilichopangwa kufanyika Jumapili, Mei Mosi 2016, kimeahirishwa hadi Jumanne Mei 3, mwaka huu.

Sababu za kuahirisha kikao hicho ni kwamba baadhi ya wajumbe wamepata udhuru hivyo wangeshindwa kuhudhuria kikao hicho kitakachofanyika
jijini Dar es Salaam kupitia mashauri mbalimbali yaliyowasilishwa.  Wafuatao kesi zao sitasikilizwa katika kikao hicho:

 1. (i) John Bocco – Azam FC
 2. (ii) Shomari Kapombe – Azam FC
 3. (iii) Aishi Manula – Azam FC
 4. (iv) Amissi Tambwe – Yanga SC
 5. (v) Donald Ngoma  - Yanga SC
 6. (vi) Paulo Jinga – JKT Rwamkoma FC
 7. (vii) Kipre Tchetche – Azam FC
 8. (viii) Abel Katunda – Transit Camp
 9. (ix) Zephlyn Laurian – JKT Rwamkoma FC
 10. (x) Idrisa Mohamed – JKT Rwamkoma
 11. (xi) DR. Mganaga Kitambi (Daktari) – Coastal Union
 12. (xii) Herry Chibakasa – Friends Rangers
 13. (xiii) Ismail Nkulo – Polisi Dodoma
 14. (xiv) Said Juma – Polisi Dodoma
 15. (xv) Idd Selaman – Polisi Dodoma
 16. (xvi) Edward Amos – Polisi Dodoma
 17. (xvii) Stewart Hall (Kocha)– Azam FC
IMETOLEWA NA MSEMAJI WA TFF, ALFRED LUCAS MAPUNDA 'MAPS'

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV