April 29, 2016



Uchaguzi wa Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (Kifa) ambao ulikuwa ufanyike kesho Jumapili, umepigwa kalenda baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kumpambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kuingilia kati mchakato huo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Kifa, Samwel Ntabaliba amefunguka kuwa, wameamua kusogeza mbele uchaguzi huo ambao sasa utafanyika Mei 8, mwaka huu ili kupisha uchunguzi wa Takukuru juu ya wagombea walioenguliwa lakini wanaendelea na mchakato wenyewe.

“Uchaguzi ulikuwa ufanyike Jumapili lakini tumeamua kuusogeza kutokana na Takukuru kuingilia kati kufuatia kuhoji juu ya wagombea watatu katika nafasi ya utunza fedha ambao ni Amania Kamungu na wengine wawili wanaogombea nafasi za ujumbe ambao walienguliwa wakati mimi sipo hivyo imetaka kuhoji kwa nini wamerejeshwa katika kinyang’anyiro hicho huku wakiwa walienguliwa.

“Takukuru ilichukua simu zetu sote, sisi watu wa kamati ya uchaguzi kwa muda wa wiki moja hivyo kushindwa kujipanga katika suala zima la uchaguzi ambapo wameturejeshea Jumamosi, hivyo ndiyo sababu ya kushindwa kuandaa uchaguzi.

“Hivyo kwa misingi hiyo uchaguzi utafanyika Mei 8 na tayari nimeshaandika barua kwa uongozi wa Kifa kuwataarifu juu ya suala hilo pia nimewaandikia barua ofisi za Takukuru Kinondoni ili kujua nini tufanye kuhusiana na suala hilo kwa kujua iwapo watu hao wataenguliwa ama watabakia,” alisema Ntabaliba.


Aidha kuna madai kuwa uchaguzi huo umeshindwa kufanyika kutokana na upande wa uongozi uliopo madarakani haukujiandaa vya kutosha hivyo kuamua kuandika barua katika kamati hiyo ili uchaguzi usogezwe mbele.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic