September 19, 2016

Kiungo wa Azam FC, Himid Mao, amekubali yaishe baada ya kusema kuwa kikosi cha Simba msimu huu kipo vizuri ukilinganisha na msimu uliopita.

Mao aliyasema hayo baada ya juzi Jumamosi Simba kuitembezea kichapo cha bao 1-0 Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Championi Jumatatu, Mao alisema kuwa msimu huu kikosi cha Simba kipo vizuri na hiyo ni kutokana na usajili waliofanya.


Himid Mao

Simba ilipoumana na Azam

“Tulipambana sana uwanjani lakini mwisho wa siku Simba ndiyo walioibuka na ushindi, nawapongeza kwa hilo lakini pia nimegundua kuwa kikosi chao safari hii kipo vizuri.


“Hata hivyo tumekipokea kipigo hicho kwa mikono miwili, upungufu wote uliojitokeza katika mchezo huo, najua kocha atakuwa ameuona na ataufanyia kazi ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika mechi zetu nyingine kwa sababu kupoteza mchezo huo siyo kwamba ligi imeisha, tunatakiwa kushinda michezo yetu mingine iliyobakia,” alisema Mao.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic