September 19, 2016

Mchezo wa Mwadui dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga ulikuwa na presha kubwa kwa makocha wa timu hizo kiasi cha kusababisha kutaka kushikana wakati wa mapumziko.

SALEH JEMBE iliripoti juu ya tukio hilo juzi Jumamosi na kueleza kuwa wakati timu zikiendelea kupumzika, Kocha wa Yanga, Hans van Pluijm na Kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ walirushiana maneno kiasi cha kutaka kutupiana makonde.Kama siyo busara za wasaidizi wao basi makocha hao walikuwa na uwezo wa kushikana kabisa kwa jinsi upepo ulivyokuwa na wakati huo tayari Yanga ilikuwa ikiongoza bao 1-0 lililofungwa na Amiss Tambwe.

Lakini baada ya mchezo huo makocha hao walimaliza tofauti zao kwa kusalimiana huku wakicheka na kuzungumza kama vile hakuna kibaya kilichotokea. 

Hivyo ndivyo soka lilivyo, bravo kwa Julio na Pluijm.

1 COMMENTS:

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV