December 6, 2016



Kiongozi mmoja wa Simba, amesema hawana nia mbaya au ugomvi na nahodha wao, Jonas Mkude.

Lakini ulichoshwa na namns alivyoamua kuchukua uamuzi wa kuwakimbia kama sehemu ya kuwakomoa.

Tayari Simba iko katika mazungumzo ya mwisho ya kumsajili kiungo kinda aitwaye James Kotei raia wa Ghana.

Akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji, kiongozi huyo ambaye yuko kwenye kamati ya usajili, pia kamati ya utendaji amesema.

“Sisi ni binadamu pia na watu wanapaswa kulielewa hilo. Si watu wafanye mambo tu wakiamini sisi ni wabaya au hatuwajali wachezaji.

“Angalia mchezaji kama Mkude, tumemlea, tunaye hadi sasa. Lakini linapofika suala la kusaini mkataba anaanza kukimbia.

“Jiulize katika hali ya kawaida, mtu unayeamini ana mapenzi na klabu, vipi akimbie. Kama hataki kubaki, kwa nini asije mkaonana uso kwa uso na kusema ukweli kwamba yeye ana mpango mwingine, upo hivi na hataki kubaki.

“Kama akisema hivyo akashikilia msimamo ni rahisi kuamini. Lakini anakimbia huku akiwa amezima simu, hii ni tabia mbovu kabisa.

“Huenda kuna watu wanaamini Simba haiwezi kwenda bila ya mtu mmoja. Hili si kweli, haliwezi kuwa sahihi.
“Tumeona kuwa Mkude hataki kubaki, kwa kifupi kama viongozi tumeona tumpe nafasi na sisi tutafute mtu ambaye siku ikifika ataziba pengo lake,” alisema akionyesha wazi kuchukizwa na tabia ya Mkude kuzima simu kwa siku kadhaa wakati akiwa ameanza mawasiliano na viongozi wa Simba kwa ajili ya kuongeza mkataba.

Taarifa za awali, zilieleza Mkude alihitaji Sh milioni 80 wakati Simba ilianzia Sh milioni 50, mwisho ikakomea kwenye milioni 60 na yeye akaona hazitoshi, akazima simu.


Hata hivyo, awali pia Mkude alihojiwa na kusema aliamua kuzima simu baada ya baadhi ya ndugu kuanza kumsumbua baada ya kuzikia alishapewa fedha za usajili baada ya kiongozi mmoja wa Simba kusema wamemalizana, jambo ambalo halikuwa sahihi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic