December 6, 2016

OFISA WA STAR MEDIA LTD, JOSEPHINE JOSEPH


Huku siku zikiwa zinahesabika kuelekea kwenye Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya, Kampuni ya Star Media Limited wasambazaji wa king'amuzi maarufu cha Startimes, imeamua kuja na chemsha bongo ambayo itawafanya wateja wake wote kujishindia runinga mpya za kisasa kila siku ya Jumatano.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo, leo. Ofisa Uhusiano wa kampuni hiyo, Josephine Stephen, alisema kwamba, wameamua kuanzisha chemsha bongo hiyo ikiwa ni moja ya njia ya kuwashirikisha wateja wao kwenye msimu huu wa sikukuu.


“StarTime, imejipanga kurejesha baadhi ya faida zetu kwa wateja kupitia kampeni hii ya chemsha bongo ambayo itakuwa ikiendeshwa kwa kurushwa hewani kupitia Kituo cha Runinga cha TV1 kuanzia saa 2:00 hadi 2:15, kila siku ya Jumatano na marudio yake ni Alhamisi saa 4:00 usiku, katika kituo cha Chaneli Ten,” alisema Josephine.





Chemsha bongo hiyo itaanza rasmi Desemba 14, mwaka huu na mwisho wake itakuwa ni Januari 14, mwakani, hivyo Josephine amewataka wateja wake wote, wahakikishe wanashiriki kujibu maswali yatokanayo na bidhaa za StarTime kwa ukamilifu ili kujipatia nafasi ya kuibuka na runinga ya kisasa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic