December 6, 2016





Kiungo mpya wa Yanga, Justce Zulu ameanza kuonyesha mwanga katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea.

Zulu raia wa Zambia amejiunga na Yanga baada ya kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitano.

Lakini taratibu amekuwa akionekana kuimarika na mara kadhaa, Kocha George Lwandamina amekuwa akimhimiza kufanya kazi ya ziada.

Utoaji wa pasi,namna ambavyo amekuwa akienda na mazoezi, inaonyesha ataimarika zaidi baada ya kuanza kucheza mechi mazoezi na zile za kirafiki.


Inaelezwa Zulu ndiye atachukua nafasi ya Mbuyu Twite raia wa DR Congo.

Zulu ni chaguo la kwanza la Lwandamina ambaye amechukua nafasi ya Hans van der Pluijm.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic