February 17, 2018



Mshambuliaji Papy Kambale amerejea na kuisaidia timu yake ya singida United kupata sare ya bao 1-1 ikiwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar.

Kambare alifunga bao la kusawazisha katika dakika ya 49 baada ya Kagera kutangulia kwa mkwaju wa penalti wa Mohamed Fakhi katika dakika ya 33.

Kambale alikuwa amesimamishwa na uongozi wa Singida United baada ya kufanya vurugu katika mechi mbili.

Upande mwingine, Majimaji ikiwa ugenini ilipata sare ya 1-1 dhidi ya Njombe Mji, shujaa akiwa Aziz Sibo aliyesawazisha dakika za majeruhi.


Kabla wenyeji Njombe Mji walikuwa wamepata bao kupitia kwa Ditram Nchimbi ambaye alijiunga na Njombe akitokea Majimaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic