Vigogo wa Ujerumani, Bayern Munich usiku wa kuamkia leo Jumatano wamezidi kumuweka matatizoni zaidi Kocha Arsene Wenger kwa mashabiki wa Arsenal baada ya kuichapa timu yake mabao 3-1.
Arsenal iliyokuwa nyumbani Emirates London, ilikutana na
kipigo hicho hali inayozidi kuamsha mgogoro kati ya Wenger na mashabiki ambao
walionyesha kupoteza imani na kikosi chao hata kabla ya mechi hiyo.
Ligi ya Mabingwa ndiyo michuano pekee ambayo Arsenal
wanapambana kupata kombe baada ya kuwa wameng’olewa katika Kombe la FA baada ya
kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Blackburn Rovers.
Kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Wajerumani hao, ni sawa na
kuthibitisha kwamba Arsenal haitabeba kombe lolote katika kipindi cha miaka
nane. Labda itokee miujiza mjini Munich na wao wasonge mbele hadi katika robo
fainali.
Katika mechi ya jana, Bayern pamoja na kuwa wenyeji walicheza
kwa kujiamini zaidi na kufanikiwa kupata mabao yao mawili katika kipindi cha
kwanza kupitia Toni Kroos aliyepiga shuti katika
ya mabeki wa Arsenal katika dakika ya 7 na Thomas Muller aliyepiga la pili dakika
ya 21.
Mjerumani Lukas Podolski aliifungia
Arsenal bao pekee kwa kichwa katika dakika ya 55. Wakati Arsenal wanaonekana
kupania kusawazisha, Mario Mandzukic akawazika kwa bao la tatu katika dakika ya
77.
Mechi nyingine ya raundi ya 16 Bora
jana ilikuwa ni kati ya FC Porto ikiwa nyumbani iliizamisha Malaga ya Hispania
kwa bao 1-0 lililofungwa na Moutinho.
LEO:
AC Milan v
Barcelona
Galatasaray
v Schalke
0 COMMENTS:
Post a Comment