February 20, 2013

picha na saleh ally

Kocha Mkuu wa Recreativo Libolo amesema ni lazima waifunge Simba katika mechi ya marudiano ili kusonga mbele kwa kujiamini zaidi.

Akizungumza na mtandao wa Angolasports, Henrique Calisto amesema ana uhakika wataishinda Simba na watafanya hivyo kuifanya timu yake kuwa na uhakika zaidi.
“Ushindi unajenga hali ya kujiamini, bado Simba si timu ya kudharau lakini tunataka kushinda na si are. Tukishinda tutajiamiani na zaidi katika hatua inayofuata.
“Kitu kizuri kwetu ni kuishinda Simba itakapocheza nasi hapa Angola. Ushindi wa Dar es Salaam, bado si majibu sahihi kwetu, tumemaliza mchezo mmoja, sasa unafuata wa pili,” alisema Calisto.
Katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Libolo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufanikiwa kuonyesha soka la kuvutia dhidi ya wenyeji wake Simba.
Libolo ambao watakuwa wenyeji katika mchezo wa pili, wanahitaji sare tu ili kusonga mbele, wakati Simba wanahitaji ushindi wa zaidi ya mabao mawili halafu wasiruhusu hata bao moja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic