February 19, 2013




Mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel ametamba kuwa kikosi chake hicho cha zamani hakitatoka katika mechi ya kesho.
Simba tayari iko mjini Mbeya kuivaa Prisons katika mechi ya Ligi Kuu Bara na Gabriel maarufu kama Batigol ametamba timu yake mpya itashinda.
“Najua Simba wana kikosi kizuri, wala hatuwezi kubweteka kwa kuwa wamefungwa na Waangola.
“Lakini nakuhakikishia huku hawatatoka, wakibahatisha ni sare. Kikosi chetu kiko fiti sana,” alisema Gabriel.

Wakati Gabriel anatamba, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig anaamini watabadilika na kucheza vizuri.
“Tumeona makosa na tumeyafanyia kazi, hofu kubwa ni ubovu wa kiwanja lakini tutafanya vizuri na kushinda.
“Timu kubwa kama Simba lazima itakuwa inapaniwa, wachezaji wanalijua hilo na tutakuwa makini zaidi,” alisema Mfaransa huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic