February 19, 2013



China imewafungia maisha wachezaji na maofisa 33 kutokana na kujihusisha na masuala ya rushwa na upangaji matokeo katika ligi kuu ya nchi hiyo.
Pamoja na hivyo, timu ya zamani ya Didier Drogba ya Shanghai Shenhua imepokwa ubingwa wake iliyoubeba mwaka 2003 ikiwa ni pamoja na kupigwa faini ya yuan milioni moja (sawa na pauni 103,000) baada ya kupatikana na hatia ya upangaji matokeo.
China imekuwa ikihaha kutaka kuusafisha mchezo wa soka kutokana na kutawaliwa na vituko vya upangaji matokeo na tayari zaidi ya viongozi wa klabu na mashirikisho wapatao 50 wakiwemo waamuzi na wachezaji 50, wamefungwa jela.
Moja ya vituko vimekuwa maarufu katika ligi ya China ni kutokana na timu nyingi kutaka kujifunga mabao. Wachezaji wamekuwa wakihongwa na wacheza kamari ili wazifungishe timu zao.
Shanghai Shenhua pia ilipatikana na hatia ya kutoa rushwa katika mechi iliyoshinda kwa mabao 4-1 dhidi ya Shanxi Guoli, vyombo vya habari vya China vimeeleza hilo.
Jumla ya timu 12 pamoja na Shanghai Shenhua zimetozwa faini ya fedha au kupokwa pointi sita katika msimu ujao wa ligi hiyo.
Ukiachana na hao waliofungiwa maisha, wachezaji na viongozi 25, wenyewe wamepunguziwa adhabu kwa kufungiwa mechi tano tu.
Didier Drogba na Nicolas Anelka waliichezea Shanghai Shenhua mwaka jana kabla ya kuhamia Galatasaray na Juventus.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic