February 21, 2013



Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), leo imekabidhi basi aina ya Yutong kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya matumizi ya timu ya soka ya taifa (Taifa Stars).
Stars ambayo siku za hivi karibuni iling’ara katika mechi za kirafiki kwa kuzitwanga Zambia na Caneroon, itakuwa ikitumia basi hilo kubwa aina ya Yutong lenye thamani ya Sh milioni 200.
Pamoja na basi hilo, TBL imeongeza udhamini wake kwa Stars na jumla itakuwa Sh bilioni 4.2 badala ya ile ya Sh bilioni 3.2 ya awali.
TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro ni wadhamini wa Taifa Stars pia mabingwa wa soka Tanzania, Simba na vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga ambao wote wameshakabidhiwa basi kama hilo.
Hafla hiyo ilifanyika jana kwenye makao makuu ya TBL, Ilala jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi kutoka TBL, TFF pamoja na Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic