February 21, 2013



Amrouche

Kocha Adel Amrouche raia wa Ubeligiji ndiye kocha mpya wa timu ya soka ya taifa ya Kenya, Harambee Stars baada ya kupewa mkataba mpya.
Amrouche ambaye asili yake ni nchini Algeria aliwahi kutaka kuinoa Taifa Stars baada ya kuondoka kwa Maximo, hata hivyo juhudi zake ziligonga mwamba, kazi akapewa Jan Poulsen maarufu kama Babu.
Ntagwabira 
Mbeligiji huyo, naye amemtangaza Jean Marie Ntagwabira raia wa Rwanda ambaye aliwahi kuitaka Yanga bila ya mafanikio kuwa kocha msaidizi.
Jean Marie alikuwa kocha msaidizi wa Rwanda ‘Amavubi’ chini ya Mserbia, Sredojevich Milutin ‘Micho’ wakati Amrouche aliamua kuvunja mkataba wake wa miaka mitano kuinoa Burundi ‘Itamba Murugamba’.
Kenya ambayo imeomba kuwa mwenyeji wa Kombe la Mataifa Afrika mwaka wa miaka 2019 imeamua kuingia mkataba na Amrouche ambaye alionyesha juhudi na uchapakazi wakati akiwa na Burundi bila ya kujali shida na matatizo mengi katika kikosi hicho.
Amrouche amewapiku makocha zaidi ya 30 waliokuwa wanawania nafasi hiyo mara baada ya Mfaransa, Henri Michel kuamua kuachia ngazi.
Kwa upande wa klabu Amrouche aliwahi kung’ara na DC Motema Pembe ya DR Congo wakati Jean Marie alifanya vizuri na APR na baadaye Atraco zote za Rwanda ambazo alizipa ubingwa wan chi hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic