February 21, 2013





MAMBO yanaweza yakaenda kuliko yalivyotegemewa kwa Kocha wa zamani wa Simba, Milovan Cirkovic kulipwa fedha zake ndani ya saa 48, awali ilikuwa hadi Jumapili ndiyo malipo yangekuwa yamekamilika.

Mlezi wa Simba, Rahma Al Kharusi amethibitisha kwamba tayari yuko jijini Muscat, Oman na ameanza kulishughulikia suala la Milovan.

“Huenda ikawa mapema zaidi, tayari nimeanza kufanya mchakato, hadi leo mchana huu (Alhamisi) nitakuwa nimepiga hatua.

“Ingawa nimebanwa na mambo yangu mengine, lakini nitajitahidi kulimaliza ndani ya leo na kesho na kocha atakuwa ameshapata fedha zake,” alisema Rahma ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa kamati ya fedha ya Simba.

Malkia wa nyuki aliamua kuingilia na kutangaza kumlipa Milovan fedha dola 32,000 anazowadai Simba ambazo zilitokana na mishahara yake minne.
Tokea ametua nchini, hakuna kiongozi hata mmoja wa Simba aliinua mguu wake na kumfuata kwa ajili ya mazungumzo.

Badala yake, wengi walikuwa wakimuona Uwanja wa Taifa jijini Dar alipokuwa anakwenda kushuhudia mechi mbalimbali za ligi ikiwemo ila kati ya Simba dhidi ya Libolo.

Katika mechi hiyo Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage alimfuata na kumyanyua mkono akionyesha wako pamoja naye, lakini mashabiki wakamzomea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic