February 19, 2013




Fanja FC ya Oman ambao walikuwa wenyeji wa Simba wakati wa kambi yao nchini humo, wamepigwa 5-0.
Fanja ambao wanatarajia kuja nchini kwa ajili ya kufanya maandalizi ya msimu ujao, baada ya kupokea kipigo hicho tayari wamemtimua kocha mkuu na msaidizi wake.
Taarifa zinaeleza, tayari mchakato wa kumsaka kocha mpya kwa ajili ya kuziba nafasi iliyoachwa na kocha huyo.
Fanja na Oman Club ndiyo timu kubwa za Oman kama ilivyo kwa Yanga na Simba nchini Tanzania.
Wakati Simba ikiwa Muscat, hawakufanikiwa kucheza na Simba kutokana na kutoa wachezaji tisa katika timu ya taifa ya jeshi ambayo ilicheza na kuifunga Simba 3-1.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic