Siku
ya kumaliza ubishi imewadia, Yanga v FC Azam katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mechi
hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu, leo ndiyo siku ya kumaliza ubishi, raha
kila timu ina pointi 36 ingawa Azam wana mchezo mmoja zaidi waliocheza.
Ushindi
ni kitu muhimu kwa kila upande, lakini kuna mengi ya kujiuliza kwamba itakuwa
vipi?
TAKWIMU:
Takwimu
zinaonyesha timu zote mbili hazina tofauti kubwa katika mambo mengi muhimu,
mfano ukiangalia mechi za mwisho Yanga ilishinda 4-0 dhidi ya African Lyon na
Azam FC ikashinda kwa idadi hiyo dhidi ya Ruvu JKT.
Yanga
imeshinda mechi 11 na kupoteza mbili, ina sare tatu wakati Azam FC pia
imeshinda 11, imepoteza tatu na sare tatu.
KUFUNGA&KUFUNGWA:
Yanga
imefunga mabao 33 na kufungwa 12 na kuifanya safu yake ya ulinzi kuwa imara
zaidi hadi sasa na Azam FC imefunga mabao 31 na kufungwa 14, unaweza kusema
hata wao safu yao ya ulinzi bado ni imara.
VIUNGO:
Viungo
wa timu zote mbili watakuwa kivutio leo, Yanga ikiwategemea zaidi Athuman Idd ‘Chuji’
na kiungo nyota kutoka Rwanda, Haruna Niyonzima. Lakini Azam FC wana Humphrey
Mieno, Ibrahim Mwaipopo na kiungo mtaalamu wa Kitanzania, Salum Abubakari ‘Sure
Boy’.
WASHAMBULIAJI:
Kila
upande una washambuliaji hatari, John Bocco amerejea dimbani, ni mwiba mkali
kwa Yanga lakini wana Mganda, Brayan Umonyi pamoja na makinda wawili hatari, Hamis
Mcha na Seif Abdallah.
Kiongozi
wa mashambulizi hayo atakuwa Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast ambaye anaongoza
listi ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara kwa kuwa na mabao 10 akifuatiwa na
Didier
Kavumbagu wa Yanga mwenye tisa.
Yanga
pia ina hazina ya watikisa nyavu kama Kavumbagu, Jerry Tegete, Said Bahanuzi na
Hamis Kiiza na kocha wao, Ernie Brandts atakuwa na kazi ya kuchagua ingawa
inaonekana lazima ataanza na Tegete ambaye sasa yuko ‘on fire’.
WAKONGWE:
Kila
upande una wakongwe na hawapaswi kudharauliwa, Nizar Khalfan kwa Yanga na
Gaudence Mwaikimba na Abdi Kassim ''Babi' kutoka Azam FC.
Bado
ni wachezaji wenye uwezo na wakati mwingine wanakuwa bora zaidi katika mechi
ngumu kama hizo.
Inawezekana
kabisa, mwamuzi wa mechi ya leo analazimika kutulia zaidi ili adhibiti mchezo
na kuondoa hisia kwamba kuna upande unaweza ukawa umecheza game hata kabla ya
kuingia uwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment