Pikipiki iliyobuniwa na
mshambuliaji nyota wa Man United, Wayne Rooney imeuzwa kwa kitita cha pauni
43,000 (zaidi ya Sh milioni 90).
Pikipiki hiyo imebuniwa na
Rooney mwenyewe baada Lauge Jensen raia wa Denmark kumshauri Rooney kufanya
hivyo kwa ajili ya kuiza ili kusaidia mambo mbalimbali ya jamii hasa watoto
wenye matatizo.
Hata hivyo, mauzo hayo ya
pauni 43,000 ya pikipiki hiyo yenye kasi ya 155 kwa saa yalikuwa pungufu pauni
15,000 tofauti na makadirio ya awali.
Hata hivyo pikipiki hiyo
iliyobuniwa na Rooney mwenye miaka 27, imekuwa kivutio kwa wengi na huenda
zinaendelea kupata soko na kumsaidia kuingiza mamilioni hya fedha.
Wakati wa
kubuni, Rooney alitumua mfano wa picha yake wakati akishangilia baada ya
kufunga bao la tik-tak katika mechi dhidi ya wapinzani wao wakubwa Man City,
mwaka 2001.
Inaaminika kilichosababisha pikipiki hiyo kununuliwa kwa bei ya chini ni Rooney kushindwa kuwashawishi wateja, kwani awali walitegemea inunuliwe kwa pauni 56,000 kwani mara nyingi pikipiki za Lauge Jensen zimekuwa zikinunuliwa hadi pauni 60,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment