Kocha wa Polisi
Morogoro, Adolf Rishard ndiye ameng’ara zaidi katika mzunguko wa pili hasa
mechi zilizochezwa mwishoni mwa mwezi uliopita na mwanzoni mwa mwezi huu.
Rishard aliyewahi
kung’ara wakati akiwa mchezaji, ameiongoza Polisi Morogogo kushinda mechi tatu
mfululizo ikiwa ni pamoja na kutoka sare na Azam FC kwa kufungana nayo bao 1-1.
Pamoja na kwamba
Azam FC imekuwa ni mwiba kwenye Uwanja wa Chamazi Complex inaoumiliki, lakini
kikosi cha Rishard kilionyesha ni imara na kupata sare hiyo.
Azam FC imekuwa
hatari inapokuwa kwenda dimba hilo, kwani hivi karibuni pamoja na Mtibwa Sugar
kuzisumbua Yanga na Simba katika mechi nne ilizocheza nazo bila ya kupoteza
hata moja, ilijikuta ‘ikilamba’ bao 4-0 kutoka kwa Azam kwenye uwanja huo.
Wakati Polisi Moro
inaonkena inapigania maisha kutokana na kuwa mkiani, lakini iliweza kupata sare
hiyo huku ikionyesha soka ya kuvutia chini ya uongozi wa kocha huyo msaidizi wa zamani wa Twiga Stars.
Polisi Moro
imeshinda mechi tatu tu baada ya kucheza 20, imefunga mabao 10 na kufungwa 19
huku ikiwa pointi 17 katika nafasi ya 12 kati ya timu 14 za ligi hiyo.
Rishard alitua
Polisi Moro kuchukua nafasi ya mkongwe mwingine, John Simkoko baada ya kuingoza
timu hiyo mechi 13 za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Bara bila ya ushindi hata
mmoja.
0 COMMENTS:
Post a Comment