Beki matata wa
Barcelona, Dani Alves amewashukia mashabiki wa wapinzani wao Real Madrid na
kusema hajali hata kidogo chuki zao.
Alves ameliambia
jarida maarufu la El Mundo kuwa, wala hajawahi kukosa usingizi kutokana na
kuchukiwa na mashabiki wa Madrid kwa kuwa angekuwa anachezea timu hiyo, huenda
wale wa Barcelona pia wangemchukia.
“Ni kitu cha
kawaida kabisa, kamwe siwezi kuinua mdomo kuwaomba wasinichukie. Wanajua wanachokifanya
nami naijua kazi yangu.
“Inawezekana hata
wa Barcelona wangeweza kunichukia kama ningekuwa nachezea Real Madrid,
ukiangalia vizuri ndiyo mambo ya soka,” alisema alves raia wa Brazil.
Alipoulizwa kuhusiana
na Barcelona kupoteza mvuto kama ilivyokuwa awali hasa kuhusiana na uchezaji
wake.
Alves alikiri kuwa
na mabadiliko na Barcelona kutocheza soka lake, lakini akasisitiza tayari
kikosi chao kimerejea katika kiwango chake na itaanza kuonyesha makali katika
mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AC Milan, baada ya kuwa
imelala kwa mabao 2-0 ugenini nchini Italia katika mechi ya kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment