Simba imepanga
kutuma wajumbe nchini Tunisia kwenda kufuatilia malipo ya kiungo mshambuliaji
wake wa zamani, Emmanue Okwi.
Wanachotaka Simba
ni kulipwa fedha zao dola 300,000 au warudishiwe Okwi na tayari wamepeleka
maombi yao kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuhusiana na hilo.
Lakini rafiki wa
karibu wa Okwi, amesema kamwe Mganda huyo hatakubaliana na hilo la kurejea
nchini na kuichezea Simba, badala yake wao ndiyo wamalizane na klabu yake mpya
ya Etoile du Sahel.
“Tayari Okwi
anajua kila kitu, lakini kaniambia kamwe hawezi kuthubutu kurejea Tanzania kwa
kuwa alishamalizana vizuri na Simba pamoja na Etoile du Sahel ambayo ilimlipa
fedha yake.
“Hivyo anaona ni
vizuri aendelee kubaki hapo huku akijaribu kupambana na maisha,” alisema rafiki
huyo.
Pamoja na rafiki
yake huyo kusema hiyo, inaonekana ni vigumu kwa Okwi iliyeelezwa analipwa
mshahara wa dola 15,000 kurejea nchini kuchukua dola 1,200 aliyokuwa akilamba
Simba.
Okwi bado hajapata
namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, lakini amekuwa akiendelea mazoezi
na wenzake wa kikosi cha kwanza huku akionekana kuwa na nyuso ya furaha.
Etoile du Sahel
iliahidi kuilipa Simba fedha hizo za usajili kwa mafungu mawili, lakini
haikutekeleza suala hilo na imekuwa ikiendelea kupiga kalenda.
Imeelezwa, Simba
wamemuomba Malkia wa Nyuki ambaye ni mlezi wao, kupanda hadi Tunisia kwenda
kulishughulikia suala hilo badala ya kuwaamini Fifa ambao wakati mwingine
wamekuwa wazito kushughulikia matatizo ya timu zisizokuwa maarufu sana.
0 COMMENTS:
Post a Comment