May 16, 2018DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA, YANGA 0-0 RAYON

Dak ya 93, Mpira utamalizika muda wowote
Dak ya 92, Kona inapigwa kuelekea Rayon, unapigwa lakini Rayon wanaokoa

DAKIKA 90 ZIMEMALIZIKA, ZIMEONGEZWA TATU

Dak ya 88, Mwashiuya ametolewa na nafasi yake imechukuliwa na Emmanuel Martin
Dak ya 87, Rayon wanakwenda langoni mwa Yanga, pigwa krosi moja hovyo inakwenda nje
Dak ya 86, Milango ni migumu
Dak ya 84, Kamusoko ametoka, nafasi yake imechukuliwa Amis Tambwe

Dak ya 80, Faulo, Rayon wanapata faulo nje kidogo ya eneo la hatari, wasipokuwa makini tunaweza andika mengine
Dak ya 75, Rayooon, wanakosa goli lingine la wazii kabisa
Dak ya  73, Mwashiuya anashindwa kuituliza pasi kutoka kwa Yondani, beki Rayon anaokoa na kupiga mbeleDak ya 72,  Rayon wanafanya mabadiliko anaingia Christ anatoka Diarra
Dak ya 70, Kwenda sasa huku Rayon, mpira unatoka nje inakuwa goli kiki

Dak ya 68, Yanga wapo ndani ya eneo la boksi la wapinzani, piga huku Chiiiirwa, inagonga mwamba
Dak ya 67, Rayon nao wanatoa, Yanga wanarusha
Dak ya 67, Dante anatoa mpira nje, Rayon wanarusha
Dak ya 64, Rayon wanakosa bao la wazi kabisa, wametengeza nafasi nzuri lakini umaliziaji umekuwa ni sifuri
Dak ya 63, Gadiel Michael, anajaribu kupiga mbele huku Rayon wanaunasa, kwenda nao mbele huku Yanga wanaokoa tena
Dak ya 62, Hatari langoni mwa Yanga, wanakoswa bao 

Dak ya 61, Yondani anacheza madhambi, mpira umesimama
Dak ya 60, Bado milango ni migumu, timu zinafanya mashambulizi ya zamu kwa zamu
Dak ya 52, Pigwa tena nyingine hukuuu, Rostand anaokoa, aasalalee
Dak ya 51,Namna gani Yanga, kidogo uwakute msala, Rayon wanakosa kucheza na nyavu zao
Dak ya 49, Yanga wanafanya shambulizi moja kali lakini linashindwa kuzaa bao
Dak ya 45 Kipindi cha pili kimeanza, mabao bado ni 0-0

DAKIKA 45 ZA KWANZA ZIMEMALIZIKA

Dak ya 45, Yanga wanaotea, dakika  moja imeongezwa kuelekea mapumziko
Dak ya 43, Milango bado ni migumu, kila timu inacheza kwa tahadhari
Dak ya 42, Yanga wanageuza kibao sasa, wanaelekeza mashambulizi kwa wapinzani, hatari huku, kipa wa Rayon anadaka 
Dak ya 41, Rayon sasa wako kulia mwa Uwanja wakielekeza mashambulizi kwa Yanga, Yanga wanaokoa
Dak ya 40, Kelvin Yondani anatoa mpira nje inakuwa kona, ni ya kwanza kwa Rayon, inapigwa fupifupi huku lakini Rayon wanapoteza
Dak ya 38, Mahadhi anafanyiwa madhambi, mpira wa adhabu unapigwa kuelekea Rayon, anapiga Mwashiuya, piga shuti lakini kipa wa Rayon anaudaka maridadi kabisa

Dak ya 37, Yanga wanatoa nje, Rayon wanarusha
Dak ya 36, Yanga wanajitahidi kusogea eneo la wapinzani wao mpaka nje ya 12 lakini umakini wa kutengeneza bao unakosekana
Dak ya 34, Mpira ni goli kiki, Yanga wanaanza upya, kwake Kamusoko, anapiga kwake Mhilu
Dak ya 32, Rayon wanajaribu shambulizi moja lakini linakuwa butu, mpira unakuwa goli kiki
Dak ya 31, Mashambulizi ya zamu kwa zamu bado yanaendelea kwa timu zote mbili

Dak ya 27, Rayon wanapasiana ndani ya 18 ya Yanga, wanakwenda, pigwa pale hatarii... Mpira unatoka nje
Dak ya 25, Hatari inatokea langoni mwa Rayon, kipa almanusra mpira umteleze mikononi, Yanga wanakosa bahati nyingie ya kupata bao
Dak ya 22, Dante anachezewa faulo, mpira unapigwa kwenda Rayon
Dak ya 22, Yanga wanaanza kutoka langoni mwao
Dak ya 21, Kamusoko sasa na mpira, piga mbele huku mpaka kwa kipa wa Rayon lakini anadaka kiulani
Dak ya 19, Yanga langoni mwa wapinzani, Rayon wanaokoa, mpira unapigwa mbele kuelekea Yanga

Dak ya 18, Yusuph Mhilu anatoa mpira nje, unarushwa kuelekea Yanga
Dak ya 17, Rayon wanapata offside ya kwanza
Dak ya 15, Yanga wanajaribu kuipenya ngome ya Rayon lakini wamekuwa wagumu kwelikweli
Dak ya 14, Bado timu zote zinacheza kwa tahadhari, mashambulizi yanaenda zamu kwa zamu
Dak ya 12, Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesimama, kiti kimekuwa cha moto
Dak ya 11, Yanga wanakimbiza kwenda mbele kwa wapinzani wao, wanaokoa
Dak ya 10, Hatari, Rayon wanatengeneza nafasi nzuri lakini inashindwa kuzaa matunda

Dak ya 7, Timu zote mbili zinacheza kwa kusomana, milango imekuwa migumu
Dak ya 5, Yanga wanajichanganya kwenye safu ya mwisho, wanashindwa kuandika bao la kwanza
Dak ya 4, Rayon wamejaribu shambulizi moja, mpira umepaa juu ya nyavu za lango la Yanga
Dak ya 3, Bado Rayon wana mpira, umetolewa na unarushwa kuelekea Yanga
Dak ya 3, Rayon wanaanza nyuma, mpira upo katika himaya yao
Dak ya 2, Mpira umeanza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga wamepata kona ya mapema lakini imeshindwa kuleta madhara

3 COMMENTS:

  1. Afadhali mbinu ya kocha imefanikiwa timu imetufutia aibu tumeambulia point 1 walau tumefikia malengo tuliyo jiwekea

    ReplyDelete
  2. Masikini yangaaa!

    Anyway, at least wataweza kushiriki mashindano ya kimataifa mwaka ujao kwa kufanikiwa kupata hiyo point moja nyumbani. Ni ahueni kubwa sana.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV