April 5, 2013


Sunzu akiwa katika mazoezi ya Bongo Movie, anamsikiliza kocha kwa umakini hasa...

Siku tatu zilizopita, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Liewig alimtimua tena mazoezini mshambuliaji wake Felix Sunzu.

Sunzu raia wa Zambia alikwenda mazoezini kwenye Viwanja vya Leaders jijini Dar ili kufanya mazoezi na ilielezwa aliruhusiwa na uongozi, lakini Liewig hakuwa na taarifa.


Hivyo akaamuru Sunzu aondoke, bila ya hiyana Mzambia huyo akaondoka na kujiunga mazoezi ya Bongo Movie yaliyokuwa kwenye uwanja wa vumbi hapohapo Leaders.

Sunzu bila ya hiyana, akaendelea kujifua kwa nguvu na timu hiyo inayojumuisha wasanii wa filamu tena kwa nidhamu ya hali ya juu.
 
Sunzu akichuana na kiungo wa Bongo Movie, MC Kenyatta..
Ukimuangalia usoni alikuwa ni mtu anayetia huruma, Liewig ambaye alionekana wazi hakujisikia vizuri kuona Sunzu akifanya mazoezi upande ule alianza kulalama.

Mara baada ya mazoezi, Mfaransa huyo alianza kulalama kwamba amedharauliwa na hakupewa taarifa huku akisisitiza hadi apate maelezo kutoka kwa Sunzu ndiyo atakubali ajiunge na timu.


Upande wa pili, Simba walikuwa wanaendelea na mazoezi...

Siku iliyofuata, Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga akasema mchezaji huyo alitakiwa kuandika barua ya kujieleza.

Sunzu ameingia katika tafrani hilo baada ya kutoweka mazoezini bila ya taarifa na kukaelezwa kwamba alikimbilia kwao Zambia lakini baadaye alidai alikuwa jijini Dar amejichimbia tu kwake eneo la Keko.
Liewig analalama mara baada ya mazoezi kwisha, kulia ni Mwandishi wa Championi, Khatim Naheka 'Ntu'...

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic