Mrembo
Fanny Neguesha ameamua kuonyesha wazi penzi lake kwa mwasoka mtukutu, Mario
Balotelli kwa kuchora tatuu inayomhusu.
Mwanamitindo
huyo wa Ubeligiji amechora alama inayoonyesha ana furaha na penzi lake kwa
Balotelli.
Neguesha ameandika ujumbe huo katika mkono wake wa kushoto kwa ndani na inaelezwa waliongozana pamoja.
Pamoja na tatuu hiyo ya kuonyesha penzi lake kwa Balotelli, Fanny ,22, pia amechora ramani ya Afrika shingoni mwake.
Balotelli aliyejiunga na AC Milan akitokea Man City kwa dau la pauni milioni 19 amekuwa akifanya vizuri baada ya kufunga mabao nane katika mechi tisa alizocheza.
Lakini penzi lake na Fanny limekuwa gumzo zaidi na wamekuwa wakionekana pamoja sehemu mbalimbali.









0 COMMENTS:
Post a Comment