April 16, 2013



 
Arsenal imelazimishwa sare ya bila kufungana na Everton kutoka jijini Liverpool.

Mchezo huo mkali wa kuvutia wa Ligi Kuu England, ulimalizika kila upande ukiwa umepoteza nafasi kadhaa.


Arsenal walionekana kushambulia zaidi, lakini mambo yalionekana kuwa magumu kwa kuwa Everton pia walikuwa imara katika kiungo na safu ya ulinzi.
Kivutio zaidi ni kwamba, Kocha Mkuu wa Man United, Alex Ferguson alikuwa uwanjani hapo kuwashuhudia Arsenal ambao atakutana nao katika mbio zake za kutwaa ubingwa.


Kutokana na sare hiyo, Arsenal iliyokuwa nyumbani Emirates jijini London, inabaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 60 wakati Everton iko katika nafasi ya sita na pointi 57.


Hata hivyo, Arsenal inakuwa imefikisha mechi 33, ambazo ni mbili zaidi ya Chelsea iliyo katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 58.

Maana yake, kama Chelsea itashinda mechi ya kesho dhidi ya Fulham itakuwa imeiondoa Arsenal katika nafasi hiyo nab ado itabaki na mechi moja kibindoni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic