Kocha Mkuu
wa Simba, Patrick Liewig amegoma kurudishwa kikosini kwa wachezaji wakongwe
wakiwemo Haruna Moshi Boban na Amir Maftah.
Kocha huyo
raia wa Ufaransa ameuambia uongozi kwamba anataka kumaliza msimu akiwa na
kikosi cha wachezaji alionao, wengi wakiwa makinda.
Mfaransa
huyo ambaye tokea ajiunge na Simba imekuwa ikienda mwendo wa kusuasua, tayari
amewasilisha ripoti yake kwa uongozi kueleza kusimamishwa kwa wachezahji hao
kwa utovu wa nidhamu.
Msemaji wa
Simba, Ezekiel Kamwaga amethibitisha Liewig kuwasilisha ripoti yake kuhusiana
na wachezaji hao.
Wachezaji
wengine waliosimamishwa ni pamoja na Juma Nyosso, Abdallah Juma na Paul
Ngalema.
Uongozi wa
Simba umesema utalijadili suala hilo na kujua kama kuna kitu cha kufanya au la.
Liewig
amekuwa akilaumiwa na wachezaji wengi kutokana na tabia yake ya kuwanunia
wachezaji hasa wanapokuwa wamekosea.
Badala ya
kumalizana nao, Liewig amekuwa akinuna na kutotaka wachezaji hao wasijumuike
katika kikosi, kitu ambacho baadhi yao wamekuwa wakilaumu na kusisitiza ingekuwa
jambo la busara kama kocha huyo angekuwa akiwaita na kutatua kinachosababisha
mgongano.







0 COMMENTS:
Post a Comment