CHELSEA V FULHAM
Chelsea
ikiwa nyumbani ilionyesha kiwango baada ya kuichapa Fulham kwa mabao 3-0 katika
mechi ya Ligi Kuu England kwenye Uwanja wake wa Stamford Brigde maarufu kama
Darajani.
Kitu kizuri
zaidi kwa Chelsea, mabao yake yote matatu yalifungwa na mabeki wake wa kati.
Luiz raia wa
Brazil alifunga bao katika dakika ya 30 na nahodha John Terry akaongeza la pili
katika dakika ya 43 na timu zikaenda mapumziko, Chelsea ikiwa mbele kwa mabao
hayo mawili.
Mara kadhaa
katika kipindi cha pili, washambuliaji wa Chelsea, Moses na Torres walipoteza
nafasi kadhaa ambazo zingezaa mabao.
Chelsea ambayo
imefudi katika nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 61, ikiwa ni moja zaidi
ya Arsenal, ilipata bao lake la tatu katika dakika ya 71 baada ya Terry
kuunganisha pasi ya kichwa kutoka kwa Torres.
MAN CITY V WIGAN
Manchester City ikiwa nyumbani ilifanikiwa kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya Wigan ambao walionyesha ni wabishi kuanzia mwanzo.
City walipata bao lao hilo katika dakika ya 83 mfungaji akiwa Carlos Tevez.
Pamoja na bao hilo, City waliendelea kufanya kazi ya ziada kwani Wigan walionyesha kiwango kizuri na kuwapa wakati mgumu mabingwa hao watetezi.
WEST HAM V MAN UNITED
Pamoja na kuwa
katika mbio za ubingwa, Man United ikiwa ugenini ilijikuta ikiwa katika wakati
mgumu sana dhidi ya wenyeji wake West Ham.
West Ham
walianza kufunga bao mapema kupitia Vaz Te katika dakika ya 16, lakini Valencia
akaisawazishia Man United katika dakika ya 31 na matokeo hayo yakadumu hadi
mapumziko.
Kipindi cha
pili, Diame aliipatia bao West Ham katika dakika ya 55 na Man Unite
wakasawazisha kupitia van Persie katika dakika ya 76 ingawa bao hilo lilielezwa
kuwa ni offside.
Picha zinaonyesha
kabla ya kufunga bao hilo, van Persie alikuwa mbele ya mabeki wa West Ham,
hivyo alikuwa ameotea.

















0 COMMENTS:
Post a Comment