KOCHA Mkuu wa Simba,
Patrick Liewig, amemtaka mshambuliaji wake Mzambia, Felix Mumba Sunzu aandike
barua ya kujieleza.
Liewig raia wa Ufaransa
amemtaka Sunzu ajieleze kwa nini alitoweka mazoezini bila ya taarifa.
Sunzu amekuwa akijifua
kivyake takribani wiki mbili sasa baada ya kocha huyo kumfukuza mazoezini baada
ya kutoweka kwa siku kadhaa bila ya kumtaarifu na baadaye ikaelezwa alikwenda
kwao Zambia.
Sunzu ambaye amekuwa
akikanusha kwamba alikwenda Zambia, amekuwa katika wakati mgumu dhidi ya kocha
huyo.
Kumekuwa hakuna uelewano
mzuri kati ya Sunzu na Liewig na Mzambia huyo tayari ameweka wazi kwamba hana
raha tena ndani ya Simba.
Juzi, Liewig alimfukuza
tena Sunzu katika mazoezi ya Simba katika viwanja vya Leaders jijini Dar.
Baada ya kufukuzwa, Sunzu
alikwenda kwenye uwanja mwingine wa eneo hilo na kujiunga na timu ya waigiza
filamu maarufu kama Bongo Movie na kufanya nao mazoezi.
Tayari mshambuliaji
mwingine, Abdallah Juma ameambiwa pia aandike barua kujieleza.
Liewig aliamua kuwatosa
wakali hao na badala yake kutumia wachezaji makinda ingawa mwendo wa Simba
umekuwa haueleweki.
0 COMMENTS:
Post a Comment