Pamoja na msimamo wa
uongozi kuwasimamisha wachezaji wakongwe katika kikosi cha Simba, lakini hali
imezidi kuonekana kuwa ngumu.
Uthibitisho wa hilo
umeonekana baada ya uongozi wa Simba kuamua kumrejesha kiungo wake Mwinyi
Kazimoto.
Msemaji wa Simba, Ezekiel
Kamwaga amethibitisha uamuzi wa uongozi kumrudisha kiungo huyo kundini.
“Tayari Kazimoto amepewa
barua na ataanza mazoezi na wenzake mara moja,” alisema.
Wiki iliyopita, Kocha
Mkuu wa Simba, Patrick Liewig alizuia Kazimoto asisafiri hadi Bukoba kuungana
na kikosi hicho.
Kazimoto aliyekuwa
amemaliza majukumu ya kuichezea Taifa Stars dhidi ya Morocco alilazimika kubaki
jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment