Maisha ni kama safari isiyokuwa na mwanga, wakati
mwingine hujui baadaye mambo yatakuwa vipi.
Angalia picha hii, wachezaji wawili wa Yanga, Fred
Felix Minziro maarufu kama Baba Issaya, alikuwa beki mbili na Lawrence
Mwalusako alikuwa namna nne tegemeo.
Katika picha hii, Mizinro wa kwanza kushoto sasa ni
kocha msaidizi wa Yanga, halafu patna wake katika kikosi enzi hizo, Mwalusako (wa
nne kutoka kushoto) ni bosi wake kwa kuwa ni katibu mkuu.
Hivyo Minziro anapokwama masuala ya mshahara,
lazima amuone Mwalusako ili kurekebisha mambo.
Hatujui hua anamuitaje, labda :”Mwana rekebisha”,
au “Bosi nimekwama, jitahidi tulipwe mapema” au inawezekana kama zamani vile, :
“Babu vipi, fanya mshahara fasta, ohooo”.
Wachezaji wengine wawili katika picha hii ni Yusuf
Bana wa pili kushoto, anafuatiwa na Omar Hussein ‘Keegan’ halafu Edgar Fongo ni
baada ya Mwalusako.








0 COMMENTS:
Post a Comment